Quran with Swahili translation - Surah Maryam ayat 9 - مَريَم - Page - Juz 16
﴿قَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٞ وَقَدۡ خَلَقۡتُكَ مِن قَبۡلُ وَلَمۡ تَكُ شَيۡـٔٗا ﴾
[مَريَم: 9]
﴿قال كذلك قال ربك هو علي هين وقد خلقتك من قبل ولم﴾ [مَريَم: 9]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Malaika akasema kumjibu Zakariyyā juu ya kile alichokionea ajabu, «Mambo ni kama unavyosema kuwa mke wako ni tasa na kuwa wewe umefikia upeo wa uzee, lakini Mola wako Amesema, ‘Kumuumba Yah,yā kwa namna hii ni jambo sahali na pesi kwangu.’» Kisha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Alimtajia Zakariyyā jambo la ajabu zaidi kuliko lile aliloliuliza akasema, «Na nimekuumba wewe kabla ya Yah,yā na hukuwa ni kitu chenye kutajika wala kilichoko.» |