Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 154 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَلَا تَقُولُواْ لِمَن يُقۡتَلُ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمۡوَٰتُۢۚ بَلۡ أَحۡيَآءٞ وَلَٰكِن لَّا تَشۡعُرُونَ ﴾
[البَقَرَة: 154]
﴿ولا تقولوا لمن يقتل في سبيل الله أموات بل أحياء ولكن لا﴾ [البَقَرَة: 154]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wala msiseme, enyi Waumini, kuhusu wale wanaouawa hali ya kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kuwa wao wamekufa. Bali wao wako hai, uhai maalumu unaowahusu wao, ndani ya Makaburi yao. Wala hakuna anayejua yako vipi maisha hayo isipokuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, lakini nyinyi hamuyahisi maisha hayo. Katika haya, pana ushahidi kwamba kuna neema za kaburini |