×

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa. Lakini mwenye kufanya 2:203 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:203) ayat 203 in Swahili

2:203 Surah Al-Baqarah ayat 203 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 203 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿۞ وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ فِيٓ أَيَّامٖ مَّعۡدُودَٰتٖۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوۡمَيۡنِ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۖ لِمَنِ ٱتَّقَىٰۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ ﴾
[البَقَرَة: 203]

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa. Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kumchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake

❮ Previous Next ❯

ترجمة: واذكروا الله في أيام معدودات فمن تعجل في يومين فلا إثم عليه, باللغة السواحيلية

﴿واذكروا الله في أيام معدودات فمن تعجل في يومين فلا إثم عليه﴾ [البَقَرَة: 203]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na mtajeni Mwenyezi Mungu kwa kuleta Tasbihi na Takbiri, katika siku chache, nazo ni siku za tshrīq: siku ya kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu za mwezi wa Mfungotatu.Atakaye kufanya haraka kuondoka Mina kabla ya kutwa jua la siku ya kumi na mbili, baada ya kurusha vjiwe, hana makosa. Na yule atakaye kuchelewa kwa kulala Mina kungojea mpaka arushe vijiwe siku ya kumi na tatu, pia hana makosa, kwa aliyemcha Mwenyezi Mungu katika Hija yake. Na kuchelewa ni bora zaidi, maana huko ni kujiongezea mapato katika ibada na kufuata kitendo cha Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Na muogopeni Mwenyezi Mungu, enyi Waislamu, na mumweke mbele katika amali zenu zote; na mjue kwamba nyinyi kwake Yeye Peke Yake mtakusanywa baada ya kufa kwa ajili ya kuhesabiwa na kulipwa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek