Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 243 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿۞ أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ خَرَجُواْ مِن دِيَٰرِهِمۡ وَهُمۡ أُلُوفٌ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِ فَقَالَ لَهُمُ ٱللَّهُ مُوتُواْ ثُمَّ أَحۡيَٰهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشۡكُرُونَ ﴾
[البَقَرَة: 243]
﴿ألم تر إلى الذين خرجوا من ديارهم وهم ألوف حذر الموت فقال﴾ [البَقَرَة: 243]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hujui, ewe Mtume, kisa cha waliokimbia kutoka ardhi yao na nyumba zao, wakiwa ni maelfu mengi, wakiogopa kufa kwa sabababu ya janga la ugonjwa hatari au vita, Mwenyezi Mungu Akawaambia, «Kufeni», wakafa, papo hapo, kwa mara moja, ikiwa ni adhabu kwao kwa kukimbia kadara ya Mwenyezi Mungu, kisha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Akawahuisha baada ya muda kupita, ili waukamilishe muda wa uhai wao, na ili wapate kuwaidhika na kutubia? Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa kwa watu, kwa neema zake nyingi, lakini watu wengi hawazishukuru fadhila za Mwenyezi Mungu zilio kwao |