Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 41 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَءَامِنُواْ بِمَآ أَنزَلۡتُ مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَكُمۡ وَلَا تَكُونُوٓاْ أَوَّلَ كَافِرِۭ بِهِۦۖ وَلَا تَشۡتَرُواْ بِـَٔايَٰتِي ثَمَنٗا قَلِيلٗا وَإِيَّٰيَ فَٱتَّقُونِ ﴾
[البَقَرَة: 41]
﴿وآمنوا بما أنـزلت مصدقا لما معكم ولا تكونوا أول كافر به ولا﴾ [البَقَرَة: 41]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na iaminini Qur,ani, enyi wana wa Isrāīl, ambayo niliiteremsha kwa Muhammad, aliye Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye, ambayo inalingana na yale mnayoyajua yaliyo sahihi katika Taurati. Na msiwe ni kundi la mwanzo la Watu wa Kitabu (ahl al-kitāb) kuikanusha. Na wala msizibadilishe aya zangu kwa thamani chache ya taka za dunia zenye kuondoka. Na Kwangu Mimi, Peke Yangu, fanyeni vitendo vya kunitii na acheni kuniasi |