Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 42 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَلَا تَلۡبِسُواْ ٱلۡحَقَّ بِٱلۡبَٰطِلِ وَتَكۡتُمُواْ ٱلۡحَقَّ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ﴾
[البَقَرَة: 42]
﴿ولا تلبسوا الحق بالباطل وتكتموا الحق وأنتم تعلمون﴾ [البَقَرَة: 42]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wala msichanganye haki niliyowafafanulia, na batili mliyoizusha. Na jihadharini kuificha haki iliyo wazi ya sifa za Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ambazo zimo ndani ya vitabu vyenu. Na nyinyi mnazipata hizo zimeandikwa kwenu, katika vitabu mnavyovijua vilivyoko mikononi mwenu |