Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 55 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَإِذۡ قُلۡتُمۡ يَٰمُوسَىٰ لَن نُّؤۡمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى ٱللَّهَ جَهۡرَةٗ فَأَخَذَتۡكُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ ﴾
[البَقَرَة: 55]
﴿وإذ قلتم ياموسى لن نؤمن لك حتى نرى الله جهرة فأخذتكم الصاعقة﴾ [البَقَرَة: 55]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Kumbukeni pindi mliposema, “Ewe Mūsā! Hatutakuamini kuwa maneno tunayoyasikia kutoka kwako ni maneno ya Mwenyezi Mungu mpaka tumuone Mwenyezi Mungu waziwazi,” ukashuka moto kutoka mbinguni, na nyinyi mnauona kwa macho yenu, ukawaua kwa sababu ya madhambi yenu na ujasiri wenu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka |