Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 96 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَلَتَجِدَنَّهُمۡ أَحۡرَصَ ٱلنَّاسِ عَلَىٰ حَيَوٰةٖ وَمِنَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمۡ لَوۡ يُعَمَّرُ أَلۡفَ سَنَةٖ وَمَا هُوَ بِمُزَحۡزِحِهِۦ مِنَ ٱلۡعَذَابِ أَن يُعَمَّرَۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ ﴾
[البَقَرَة: 96]
﴿ولتجدنهم أحرص الناس على حياة ومن الذين أشركوا يود أحدهم لو يعمر﴾ [البَقَرَة: 96]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na utajua tena utajua, ewe Mtume, kuwa Mayahudi ni wenye kupenda mno, miongoni mwa watu, maisha marefu, hata yawe ni maisha ya unyonge na udhalilifu namna gani. Kupenda kwao maisha marefu kunazidi vile washirikina wanavyoyapenda. Myahudi anatamani lau ataishi miaka elfu moja. Na umri huo, lau aufikia, hautamwepusha na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, hakuna kitu chochote chenye kufichika Kwake katika matendo yao, na Atawalipa, kwa hiyo matendo yao, adhabu wanayostahiki |