Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 98 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿مَن كَانَ عَدُوّٗا لِّلَّهِ وَمَلَٰٓئِكَتِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَجِبۡرِيلَ وَمِيكَىٰلَ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَدُوّٞ لِّلۡكَٰفِرِينَ ﴾
[البَقَرَة: 98]
﴿من كان عدوا لله وملائكته ورسله وجبريل وميكال فإن الله عدو للكافرين﴾ [البَقَرَة: 98]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenye kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu, Malaika Wake, Wajumbe Wake ambao ni Malaika au binadamu, hasahasa Malaika wawili: Jibrili na Mikaili, huwa amemfanyia uadui Mwenyezi Mungu. Sababu Mayahudi walidai kwamba Jibrili ni adui wao na Mikaili ni rafiki yao. Mwenyezi Mungu Akawajulisha kwamba mwenye kuwa adui wa mmoja katika wao huwa ni adui wa Mwengine na pia ni adui wa Mwenyezi Mungu. Kwani Mwenyezi Mungu ni adui wa wenye kuyakanusha yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake Muhammad, rehema na amani zimshukie |