Quran with Swahili translation - Surah Al-Anbiya’ ayat 97 - الأنبيَاء - Page - Juz 17
﴿وَٱقۡتَرَبَ ٱلۡوَعۡدُ ٱلۡحَقُّ فَإِذَا هِيَ شَٰخِصَةٌ أَبۡصَٰرُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يَٰوَيۡلَنَا قَدۡ كُنَّا فِي غَفۡلَةٖ مِّنۡ هَٰذَا بَلۡ كُنَّا ظَٰلِمِينَ ﴾
[الأنبيَاء: 97]
﴿واقترب الوعد الحق فإذا هي شاخصة أبصار الذين كفروا ياويلنا قد كنا﴾ [الأنبيَاء: 97]
Abdullah Muhammad Abu Bakr hapo Siku ya Kiyama itakuwa imekaribia na vituko vyake vitajitokeza, na hapo utayaona macho ya makafiri yamekodoka hayapepesi kwa kibabaiko kikali, huku wakiwa wanajiapiza maangamivu kwa majuto wakisema, «Ee ole wetu! Kwa hakika tulikuwa tumeghafilika na Siku hii na kujiandalia nayo na kwa hivyo tulikuwa madhalimu.» |