Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 73 - الحج - Page - Juz 17
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٞ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُۥٓۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَن يَخۡلُقُواْ ذُبَابٗا وَلَوِ ٱجۡتَمَعُواْ لَهُۥۖ وَإِن يَسۡلُبۡهُمُ ٱلذُّبَابُ شَيۡـٔٗا لَّا يَسۡتَنقِذُوهُ مِنۡهُۚ ضَعُفَ ٱلطَّالِبُ وَٱلۡمَطۡلُوبُ ﴾
[الحج: 73]
﴿ياأيها الناس ضرب مثل فاستمعوا له إن الذين تدعون من دون الله﴾ [الحج: 73]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi watu! Kumepigwa mfano, usikilizeni na muuzingatie: Kwa hakika, masanamu na wanaodaiwa kufanana na Mwenyezi Mungu mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, hawatoweza lau wakikusanya kuumba nzi mmoja, basi itakuaje kuumba kikubwa zaidi? Wala hawawezi kukirudisha kitu alichokinyakua nzi kutoka kwao, Je kuna kuelemewa zaidi kuliko huko? Vyote viwili pamoja ni vinyonge: amedhoofika mtaka kurudisha kitu kilichochukuliwa na nzi kutoka kwake, naye ni yule muabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, na pia amedhoofika mtakwa, naye ni nzi. Basi vipi hawa masanamu na wanaofanywa kuwa wanafanana na Mwenyezi Mungu watafanywa ni waungu, ilhali wao wako kwenye udhaifu huu |