Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 8 - النور - Page - Juz 18
﴿وَيَدۡرَؤُاْ عَنۡهَا ٱلۡعَذَابَ أَن تَشۡهَدَ أَرۡبَعَ شَهَٰدَٰتِۭ بِٱللَّهِ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ ﴾
[النور: 8]
﴿ويدرأ عنها العذاب أن تشهد أربع شهادات بالله إنه لمن الكاذبين﴾ [النور: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kwa ushahidi wake huu, itapasa kwa yule mke aliyetuhumiwa kutiwa adabu ya uzinifu, nayo ni kupigwa mawe mpaka kufa. Na haitamuepukia adabu hii mpaka atoe ushahidi wa kupinga ule ushahidi wa mumewe, mara nne kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba mumewe ni mrongo katika madai yake kuwa yeye amezini |