Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 59 - النَّمل - Page - Juz 19
﴿قُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ وَسَلَٰمٌ عَلَىٰ عِبَادِهِ ٱلَّذِينَ ٱصۡطَفَىٰٓۗ ءَآللَّهُ خَيۡرٌ أَمَّا يُشۡرِكُونَ ﴾
[النَّمل: 59]
﴿قل الحمد لله وسلام على عباده الذين اصطفى آلله خير أما يشركون﴾ [النَّمل: 59]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, «Sifa njema na shukrani ni za Mewenyezi Mungu, na amani kutoka Kwake na usalama ziwashukie waja Wake Aliowateua kwa kuwapa utume.» Kisha waulize washirikina wa watu wako, «Je, Mwenyezi Mungu Anayemiliki kunufaisha na kudhuru ni bora au ni yule wanayemshirikisha badala Yake kati ya wale wasiojimilikia wenyewe wala kuwamilikia wengine nafuu yoyote wala madhara yoyote?» |