Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 48 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿فَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلۡحَقُّ مِنۡ عِندِنَا قَالُواْ لَوۡلَآ أُوتِيَ مِثۡلَ مَآ أُوتِيَ مُوسَىٰٓۚ أَوَلَمۡ يَكۡفُرُواْ بِمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ مِن قَبۡلُۖ قَالُواْ سِحۡرَانِ تَظَٰهَرَا وَقَالُوٓاْ إِنَّا بِكُلّٖ كَٰفِرُونَ ﴾
[القَصَص: 48]
﴿فلما جاءهم الحق من عندنا قالوا لولا أوتي مثل ما أوتي موسى﴾ [القَصَص: 48]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na alipowajia Muhammad watu hawa akiwa ni muonyaji kwao walisema, «Si apewe, huyu aliyetumilizwa kwetu, mfano wa kile alichopewa Mūsā, cha miujiza inayoonekana na Kitabu kilichoteremshwa mara moja.» Waambie, ewe Mtume, «Je, si Mayahudi walikikanusha kile alicholetewa Mūsā hapo kabla? Walisema kwamba ndani ya Taurati na Qur’ani kuna aina mbili za uchawi zilizosaidiana katika uchawi utokanao na hivyo viwili, na wakasema, «Sisi ni wenye kuvikanusha vyote viwili.» |