Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 17 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿إِنَّمَا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَوۡثَٰنٗا وَتَخۡلُقُونَ إِفۡكًاۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَمۡلِكُونَ لَكُمۡ رِزۡقٗا فَٱبۡتَغُواْ عِندَ ٱللَّهِ ٱلرِّزۡقَ وَٱعۡبُدُوهُ وَٱشۡكُرُواْ لَهُۥٓۖ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 17]
﴿إنما تعبدون من دون الله أوثانا وتخلقون إفكا إن الذين تعبدون من﴾ [العَنكبُوت: 17]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hamuabudu, enyi watu, badala ya Mwenyezi Mungu isipokuwa masanamu na mnazua urongo kwa kuwaita wao waungu. Kwa hakika, hawa masanamu wenu mnaoaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, hawawezi kuwaruzuku nyinyi kitu chochote, basi tafuteni riziki kwa Mwenyezi Mungu na sio kwa masanamu wenu na mumtakasie ibada na shukrani kwa kuwaruzuku. Ni kwa Mwenyezi Mungu mtarudishwa baada ya kufa kwenu, na hapo awalipe kwa yale ambayo mlifanya |