Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 38 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿وَعَادٗا وَثَمُودَاْ وَقَد تَّبَيَّنَ لَكُم مِّن مَّسَٰكِنِهِمۡۖ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ فَصَدَّهُمۡ عَنِ ٱلسَّبِيلِ وَكَانُواْ مُسۡتَبۡصِرِينَ ﴾
[العَنكبُوت: 38]
﴿وعادا وثمود وقد تبين لكم من مساكنهم وزين لهم الشيطان أعمالهم فصدهم﴾ [العَنكبُوت: 38]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tukawaangamiza kina 'Ād na Thamūd, na yameshaonekana na nyinyi magofu ya nyumba zao, vile yalivyokuwa matupu, hayana mtu yoyote katika wakazi wake, na vile mateso yetu yalivyowashukia wao wote. Na Shetani aliwapambia wao matendo yao maovu, na kwa hivyo akawazuia wasiifuate njia ya Mwenyezi Mungu na njia ya kumuamini Yeye na Mitume Wake, na walikuwa wakijiongoza kuona njia katika ukafiri wao na upotevu wao wakijifurahisha nayo, wakidhani kwamba wao wako kwenye uongofu na usawa, ilhali wao wamezama kwenye upotevu |