Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 40 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿فَكُلًّا أَخَذۡنَا بِذَنۢبِهِۦۖ فَمِنۡهُم مَّنۡ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِ حَاصِبٗا وَمِنۡهُم مَّنۡ أَخَذَتۡهُ ٱلصَّيۡحَةُ وَمِنۡهُم مَّنۡ خَسَفۡنَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ وَمِنۡهُم مَّنۡ أَغۡرَقۡنَاۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظۡلِمَهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 40]
﴿فكلا أخذنا بذنبه فمنهم من أرسلنا عليه حاصبا ومنهم من أخذته الصيحة﴾ [العَنكبُوت: 40]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kila mmoja, kati ya hao waliotajwa, tulimkamata kwa dhambi zake: kati yao kuna wale tuliyowatumia mawe ya udongo ulioshikana, nao ni watu wa Lūṭ, na kati yao kuna waliopatwa na ukelele, nao ni watu wa Ṣāliḥ na watu wa Shu'ayb , na kati yao kuna tuliowadidimiza ardhini kama vile Qārūn, na katika wao kuna tuliowazamisha majini, nao ni watu wa Nūḥ na Fir'awn na jamaa zake. Na Mwenyezi Mungu hakuwa ni Mwenye kuwaangamiza hawa kwa dhambi wengine akawa ni mwenye kuwadhulumu kwa kuwaangamiza wao bila kustahili, lakini wao walikuwa wakijidhulumu wenyewe kwa kujistarehesha kwa neema za Mola wao na kumuabudu asiyekuwa Yeye |