Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 41 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿مَثَلُ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَوۡلِيَآءَ كَمَثَلِ ٱلۡعَنكَبُوتِ ٱتَّخَذَتۡ بَيۡتٗاۖ وَإِنَّ أَوۡهَنَ ٱلۡبُيُوتِ لَبَيۡتُ ٱلۡعَنكَبُوتِۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 41]
﴿مثل الذين اتخذوا من دون الله أولياء كمثل العنكبوت اتخذت بيتا وإن﴾ [العَنكبُوت: 41]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mfano wa wale waliowafanya masanamu ni wategemewa badala ya Mwenyezi Mungu, wakawa wanatarajia msaada wao, ni kama mfano wa buibui aliyejitengenezea nyumba ili imuhifadhi, isimfalie kitu alipokuwa na haja nayo. Hivyo basi ndivyo walivyo hawa washirikina, hawakuwafalia kitu wale waliowachukuwa kuwa ni wasaidizi wao badala ya Mwenyezi Mungu. Na kwa hakika, nyumba iliyo dhaifu zaidi ni nyumba ya buibui, na lau wao wangalikuwa wakilijua hilo hawangaliwafanya wao ni wasaidizi wenye kutegemewa badala ya Mwenyezi Mungu, kwani wao hawawanufaishi wala hawawadhuru |