Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 5 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿مَن كَانَ يَرۡجُواْ لِقَآءَ ٱللَّهِ فَإِنَّ أَجَلَ ٱللَّهِ لَأٓتٖۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ﴾
[العَنكبُوت: 5]
﴿من كان يرجو لقاء الله فإن أجل الله لآت وهو السميع العليم﴾ [العَنكبُوت: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yoyote mwenye kuwa na matumaini ya kukutana na Mwenyezi Mungu na akawa na matarajio ya kupata malipo Yake mema, basi muda Aliouweka Mwenyezi Mungu wa kuwafufua viumbe Wake ili wahesabiwe na walipwe ni wenye kuja hivi karibuni. Na Yeye Ndiye Msikizi wa maneno, Mjuzi wa vitendo |