Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 8 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿وَوَصَّيۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ بِوَٰلِدَيۡهِ حُسۡنٗاۖ وَإِن جَٰهَدَاكَ لِتُشۡرِكَ بِي مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٞ فَلَا تُطِعۡهُمَآۚ إِلَيَّ مَرۡجِعُكُمۡ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 8]
﴿ووصينا الإنسان بوالديه حسنا وإن جاهداك لتشرك بي ما ليس لك به﴾ [العَنكبُوت: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tumemsihi binadamu awatendee wema wazazi wake wawili na awe mwema kwao wa maneno na vitendo. Na wakikusukuma kwa bidii, ewe binadamu, umshirikishe mwingine na mimi katika ibada yangu, basi usifuate amri yao. Matakwa ya kuwa Mwenyezi Mungu ashirikishwe yanashikanishwa na matakwa ya kuwa vitendo vingine vya maasia vifanywe. Kwani hakuna kutiiwa kiumbe namna atakavyokuwa katika jambo la kumuasi Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kama lilivyothibiti hilo kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. Kwangu mimi ndio mwisho wenu, Siku ya Kiyama, na huko niwape habari ya matendo mema na mabaya ambayo mlikuwa mkiyafanya duniani na niwalipe kwa hayo |