Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 15 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿۞ قُلۡ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيۡرٖ مِّن ذَٰلِكُمۡۖ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَأَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞ وَرِضۡوَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِٱلۡعِبَادِ ﴾
[آل عِمران: 15]
﴿قل أؤنبئكم بخير من ذلكم للذين اتقوا عند ربهم جنات تجري من﴾ [آل عِمران: 15]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema ,ewe Mtume, «Je, ni wape habari ya yaliyo bora kuliko yale waliyopambiwa watu katika maisha haya ya kilimwengu? Wale waliomchunga Mwenyezi Mungu na wakaogopa mateso Yake, watakuwa na Pepo ambazo inapita mito chini ya majumba yake ya fahari na miti yake. Watakaa milele humo. Na watakuwa nao humo wake waliotakasika na hedhi na nifasi na tabia mbaya. Na watakuwa na malipo makubwa zaidi kuliko hayo, nayo ni radhi za Mwenyezi Mungu.» Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuchungulia siri za viumbe wake, ni Mjuzi wa hali zao na atawalipa kwa hayo |