Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 163 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿هُمۡ دَرَجَٰتٌ عِندَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ ﴾
[آل عِمران: 163]
﴿هم درجات عند الله والله بصير بما يعملون﴾ [آل عِمران: 163]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Watu wa Peponi wenye kufuata yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu wanatafautiana daraja. Na watu wa Motoni wanaofuata yenye kumkasirisha Mwenyezi Mungu wanatafautiana katika matobwe. Wao hawalingani. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuziona amali zao, hakifichiki chochote Kwake katika matendo yao |