Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 17 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿ٱلصَّٰبِرِينَ وَٱلصَّٰدِقِينَ وَٱلۡقَٰنِتِينَ وَٱلۡمُنفِقِينَ وَٱلۡمُسۡتَغۡفِرِينَ بِٱلۡأَسۡحَارِ ﴾
[آل عِمران: 17]
﴿الصابرين والصادقين والقانتين والمنفقين والمستغفرين بالأسحار﴾ [آل عِمران: 17]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hawa ndio waliosifika kwa subira juu ya kumtii Mwenyezi Mungu, kuepuka maasia na juu ya shida zinazowafikia zilizokadiriwa na Mwenyezi Mungu. Na ndio waliosifika kwa ukweli wa maneno na vitendo na kutii kikamilifu. Na ndio waliosifika kwa utoaji, wa siri na wadhahiri, na kwa kuleta istighfar: kuomba msamaha, katika mwisho wa usiku, kwa kuwa wakati huo unatarajiwa zaidi kukubaliwa amali na kujibiwa dua |