Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 36 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿فَلَمَّا وَضَعَتۡهَا قَالَتۡ رَبِّ إِنِّي وَضَعۡتُهَآ أُنثَىٰ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا وَضَعَتۡ وَلَيۡسَ ٱلذَّكَرُ كَٱلۡأُنثَىٰۖ وَإِنِّي سَمَّيۡتُهَا مَرۡيَمَ وَإِنِّيٓ أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ ﴾
[آل عِمران: 36]
﴿فلما وضعتها قالت رب إني وضعتها أنثى والله أعلم بما وضعت وليس﴾ [آل عِمران: 36]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mimba yake ilipotimia na akamzaa mtoto wake alisema, «Mola wangu, mimi nimemzaa mwanamke ambaye hafai kwa kutumikia Baitulmaqdis,» Na Mwenyezi Mungu Anajua zaidi kwa alichokizaa na atamjaalia kuwa na jambo kubwa. Mke wa 'Imran aliendelea kusema, «Na Mwanamume niliyemtaka kwa kutumika si kama Mwanamke kwa hilo. Kwa kuwa mwanamume ni mwenye nguvu zaidi wa kutumika na kusimamia utumishi. Na mimi nimempa jina la Maryam. Na mimi nimemlinda kwako, yeye na watoto wake , kutokana na Shetani aliyefukuzwa kwenye rehema Yako.» |