Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 35 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿إِذۡ قَالَتِ ٱمۡرَأَتُ عِمۡرَٰنَ رَبِّ إِنِّي نَذَرۡتُ لَكَ مَا فِي بَطۡنِي مُحَرَّرٗا فَتَقَبَّلۡ مِنِّيٓۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ﴾
[آل عِمران: 35]
﴿إذ قالت امرأة عمران رب إني نذرت لك ما في بطني محررا﴾ [آل عِمران: 35]
Abdullah Muhammad Abu Bakr kumbuka, ewe Mtume, ilivyokuwa kuhusu mambo ya Maryam na mama yake na mtoto wake 'Īsā, amani imshukie, ili kuwarudi, kwa hayo, wale wanoadai uungu wa 'Īsā au kuwa yeye ni Mwana wa Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, aliposema mke wa 'Imran wakati aliposhika mimba, «Ewe Mola wangu, mimi nimekutakasia kilioko ndani ya tumbo langu kiwe ni chako Peke Yako kwa kutumikia Baitulmaqdis. Basi takabali kutoka kwangu. Hakika Wewe Peke Yako Ndiye Msikizi wa dua yangu, Ndiye Mjuzi wa nia yangu.» |