Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 49 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ أَنِّي قَدۡ جِئۡتُكُم بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ أَنِّيٓ أَخۡلُقُ لَكُم مِّنَ ٱلطِّينِ كَهَيۡـَٔةِ ٱلطَّيۡرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيۡرَۢا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۖ وَأُبۡرِئُ ٱلۡأَكۡمَهَ وَٱلۡأَبۡرَصَ وَأُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأۡكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ﴾
[آل عِمران: 49]
﴿ورسولا إلى بني إسرائيل أني قد جئتكم بآية من ربكم أني أخلق﴾ [آل عِمران: 49]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Atamjaalia awe Mtume kwa Wana wa Isrāīl na atawaambia wao, «Mimi nimewajia na alama kutoka kwa Mola wenu inayoonesha kuwa mimi nimetumilizwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Nayo ni kuwa nitawafanyia kwa udongo kitu chenye mfano wa ndege, nitapuliza ndani yake na kitakuwa ndege wa kikweli kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na nitamponya aliyezaliwa kipofu na mwenye barasi na nitamhuisha aliyekufa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na nitawaambia chakula mnachokula na mnachoweka akiba majumbani mwenu. Hakika katika mambo makubwa haya, ambayo hayako kwenye uwezo wa wanaadamu, pana dalili kwamba mimi ni Nabii wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, iwapo nyinyi ni wenye kuamini hoja za Mwenyezi Mungu na alama Zake, ni wenye kukiri kumpwekesha |