Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 60 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿فَٱصۡبِرۡ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞۖ وَلَا يَسۡتَخِفَّنَّكَ ٱلَّذِينَ لَا يُوقِنُونَ ﴾
[الرُّوم: 60]
﴿فاصبر إن وعد الله حق ولا يستخفنك الذين لا يوقنون﴾ [الرُّوم: 60]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi vumilia, ewe Mtume, kwa yale yanayokupata ya makero ya watu wako kwako na kukukanusha kwao, kwani ahadi ya Mwenyezi Mungu kwako ya ushindi, uthabiti na malipo mema ni kweli isiyo na shaka. Na wasikubabaishe wakakuweka kando na Dini yako wale wasiokuwa na yakini ya Agizo (la Siku ya Kiyama) na wasioamini kufufuliwa na malipo |