Quran with Swahili translation - Surah Luqman ayat 27 - لُقمَان - Page - Juz 21
﴿وَلَوۡ أَنَّمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن شَجَرَةٍ أَقۡلَٰمٞ وَٱلۡبَحۡرُ يَمُدُّهُۥ مِنۢ بَعۡدِهِۦ سَبۡعَةُ أَبۡحُرٖ مَّا نَفِدَتۡ كَلِمَٰتُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ ﴾
[لُقمَان: 27]
﴿ولو أنما في الأرض من شجرة أقلام والبحر يمده من بعده سبعة﴾ [لُقمَان: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau miti ya ardhi yote ingalichongwa ikafanywa kalamu na bahari ikawa ni wino wake, na zikaongezwa juu yake bahari saba, na yakaandikwa, kwa kalamu hizo na wino huo, maneno ya Mwenyezi Mungu yatokanao na ujuzi wake na hukumu Zake na yale ambayo Amewaletea wahyi Malaika Wake na Mitume Wake, zingalivunjika- vunjika kalamu hizo na ungaliisha wino huo, na hayangaliisha maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia ambayo hakuna mwenye kuyazunguka kiujuzi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mshindi Mwenye nguvu katika kuwatesa wanaomshirikisha, ni Mwingi wa hekima katika kuendesha mambo ya viumbe Vyake. Katika aya hii pana kumthibitishia Mwenyezi Mungu Aliyetukuka sifa ya Maneno kikweli, kama inavyonasibiana na utukufu Wake na ukamilifu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake |