Quran with Swahili translation - Surah Luqman ayat 29 - لُقمَان - Page - Juz 21
﴿أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلّٞ يَجۡرِيٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗى وَأَنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ ﴾
[لُقمَان: 29]
﴿ألم تر أن الله يولج الليل في النهار ويولج النهار في الليل﴾ [لُقمَان: 29]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu Anazichukua baadhi ya saa za usiku, hivyo basi mchana ukarefuka na usiku ukawa mfupi, na Anazichukua baadhi ya saa za mchana, hivyo basi usiku ukarefuka na mchana ukawa mfupi, na Amewadhalilishia jua na mwezi, kila mojawapo ya hivyo viwili kinatembea kwenye mzunguko wake hadi wakati maalumu uliopangiwa, na kwamba Mwenyezi Mungu Anayaona matendo yote ya viumbe, yawe mema au mabaya, hakuna chochote kati ya hivyo kinachofichamana Kwake |