Quran with Swahili translation - Surah As-Sajdah ayat 24 - السَّجدة - Page - Juz 21
﴿وَجَعَلۡنَا مِنۡهُمۡ أَئِمَّةٗ يَهۡدُونَ بِأَمۡرِنَا لَمَّا صَبَرُواْۖ وَكَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يُوقِنُونَ ﴾
[السَّجدة: 24]
﴿وجعلنا منهم أئمة يهدون بأمرنا لما صبروا وكانوا بآياتنا يوقنون﴾ [السَّجدة: 24]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tuliwafanya, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, ni waongozi na walinganizi kwenye wema, watu wanawafuata na wao wanawalingania kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumuabudu Peke Yake na kumtii. Na walipata daraja hii ya juu waliposubiri juu ya amri za Mwenyezi Mungu, kuyaacha makemeo Yake na kuwalingania na kuvumilia makero katika njia Yake, na walikuwa wanaziamini kikweli aya za mwenyezi Mungu na hoja Zake |