Quran with Swahili translation - Surah As-Sajdah ayat 27 - السَّجدة - Page - Juz 21
﴿أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّا نَسُوقُ ٱلۡمَآءَ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ ٱلۡجُرُزِ فَنُخۡرِجُ بِهِۦ زَرۡعٗا تَأۡكُلُ مِنۡهُ أَنۡعَٰمُهُمۡ وَأَنفُسُهُمۡۚ أَفَلَا يُبۡصِرُونَ ﴾
[السَّجدة: 27]
﴿أو لم يروا أنا نسوق الماء إلى الأرض الجرز فنخرج به زرعا﴾ [السَّجدة: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hawakuona wenye kukanusha kufufuliwa baada ya kufa kwamba sisi tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu iliyo ngumu ambayo haina mimea, tukatoa kwa maji hayo mimea yenye rangi mbalimbali yenye kuliwa na wanyama wao na miili yao ikapata chakula cha kuwafanya wao waishi kwayo? Kwani hawazioni neema hizi kwa macho yao wakajua kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwahuisha wafu na kuwafufua kutoka makaburini mwao |