Quran with Swahili translation - Surah As-Sajdah ayat 9 - السَّجدة - Page - Juz 21
﴿ثُمَّ سَوَّىٰهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِۦۖ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَۚ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ ﴾
[السَّجدة: 9]
﴿ثم سواه ونفخ فيه من روحه وجعل لكم السمع والأبصار والأفئدة قليلا﴾ [السَّجدة: 9]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kisha Aliukamilisha uumbaji wa binadamu na Akaufanya upendeze na Akalifanya zuri umbo lake, na Akapuliza ndani yake roho Yake kwa kumtuma Malaika kwake ili apulize roho, na Akawapa nyinyi, enyi watu, neema ya masikizi na maangalizi ya kupambanua sauti, rangi, vitu na watu, na neema ya akili ya kupambanua jema na baya na lenye kunufaisha na kudhuru. Ni kuchache kule kumshukuru kwenu Mola wenu kwa neema Alizowapatia |