×

Mwenyezi Mungu hakumwekea mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili 33:4 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ahzab ⮕ (33:4) ayat 4 in Swahili

33:4 Surah Al-Ahzab ayat 4 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 4 - الأحزَاب - Page - Juz 21

﴿مَّا جَعَلَ ٱللَّهُ لِرَجُلٖ مِّن قَلۡبَيۡنِ فِي جَوۡفِهِۦۚ وَمَا جَعَلَ أَزۡوَٰجَكُمُ ٱلَّٰٓـِٔي تُظَٰهِرُونَ مِنۡهُنَّ أُمَّهَٰتِكُمۡۚ وَمَا جَعَلَ أَدۡعِيَآءَكُمۡ أَبۡنَآءَكُمۡۚ ذَٰلِكُمۡ قَوۡلُكُم بِأَفۡوَٰهِكُمۡۖ وَٱللَّهُ يَقُولُ ٱلۡحَقَّ وَهُوَ يَهۡدِي ٱلسَّبِيلَ ﴾
[الأحزَاب: 4]

Mwenyezi Mungu hakumwekea mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake. Wala hakuwafanya wake zenu - ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu - kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye sema kweli, naye ndiye anaye ongoa Njia

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ما جعل الله لرجل من قلبين في جوفه وما جعل أزواجكم اللائي, باللغة السواحيلية

﴿ما جعل الله لرجل من قلبين في جوفه وما جعل أزواجكم اللائي﴾ [الأحزَاب: 4]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu hakumfanya yoyote miongoni mwa wanadamu awe na nyoyo mbili kifuani mwake, na hakuwafanya wake wenu mnaojiharamisha nao kwa njia ya ẓihār kama vile uharamu wa mama zenu. (Ẓihār ni mwanamume kumwambia mkewe, ‘Wewe ni haramu kwangu kama vile mgongo wa mamangu.’ Na hii ilikuwa ni talaka katika kipindi cha ujinga (kabla ya kuja Uislamu) na Mwenyezi Mungu Akabainisha kwamba mke hawi mama kwa namna yoyote. Na Mwenyezi Mungu Hakuwafanya watoto wa kubandika kuwa ni wana katika sheria. Bali ufananishaji na mgongo na ubandikaji wana, viwili hivyo havina uhakika katika uharamishaji wa milele, kwani mke aliyefananishwa na mgongo wa mama hawi ni kama mama katika uharamu, na nasaba haithubutu kwa kujibandika wana kwa mtu kusema kuhusu mwana wa kubandika, «Huyu ni mwanangu». Kwani haya ni maneno ya mdomo yasiyo na ukweli na hayazingatiwi. Na Mwenyezi Mungu Anasema haki na Anawabainishia waja Wake njia Yake na Anawaongoza njia ya uongofu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek