Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 3 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَا تَأۡتِينَا ٱلسَّاعَةُۖ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأۡتِيَنَّكُمۡ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِۖ لَا يَعۡزُبُ عَنۡهُ مِثۡقَالُ ذَرَّةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَآ أَصۡغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡبَرُ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ ﴾
[سَبإ: 3]
﴿وقال الذين كفروا لا تأتينا الساعة قل بلى وربي لتأتينكم عالم الغيب﴾ [سَبإ: 3]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na makafiri wenye kukanusha kufufuliwa walisema. «Kiyama hakitatujia.» Sema, ewe Mtume, uwaambie, «Kwani! Ninaapa kwa Mola wangu, kitawajia! Lakini hakuna yoyote anayejua wakati wa kuja kwake isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mjuzi wa visivyoonekana, Ambaye haufichamani Kwake uzito wa kadiri ya chungu mdogo uliyo mbinguni au ardhini, hata mdogo zaidi kuliko huo na hata mkubwa, isipokuwa uko kwenye Kitabu kilichotunzwa, nacho ni Ubao Uliohifadhiwa |