Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 33 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿وَقَالَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ بَلۡ مَكۡرُ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ إِذۡ تَأۡمُرُونَنَآ أَن نَّكۡفُرَ بِٱللَّهِ وَنَجۡعَلَ لَهُۥٓ أَندَادٗاۚ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۚ وَجَعَلۡنَا ٱلۡأَغۡلَٰلَ فِيٓ أَعۡنَاقِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۖ هَلۡ يُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ﴾
[سَبإ: 33]
﴿وقال الذين استضعفوا للذين استكبروا بل مكر الليل والنهار إذ تأمروننا أن﴾ [سَبإ: 33]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Watasema waliofanywa wanyonge kuwaambia wakubwa wao katika upotevu, «Bali ni kule kutupangia kwenu ubaya usiku na mchana ndiko kulikotutia sisi katika majanga. Kwa kuwa mlikuwa mkitutaka tumkanushe Mwenyezi Mungu na tumfanye kuwa ana washirika katika kuabudiwa.» Na watu wa kila mojawapo ya makundi mawili wataficha majuto watakapoiona adhabu ilioandaliwa wao. Na tutaweka minyororo kwenye shingo za wale waliokanusha. Na wao hawatateswa kwa adhabu hii isipokuwa ni kwa sababu ya kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu na kufanya kwao matendo mabaya duniani. Katika hii aya kuna onyo kali dhidi ya kuwafuata walinganizi wa upotevu na viongozi wa ukiukaji Sheria |