Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 39 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿قُلۡ إِنَّ رَبِّي يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦ وَيَقۡدِرُ لَهُۥۚ وَمَآ أَنفَقۡتُم مِّن شَيۡءٖ فَهُوَ يُخۡلِفُهُۥۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلرَّٰزِقِينَ ﴾
[سَبإ: 39]
﴿قل إن ربي يبسط الرزق لمن يشاء من عباده ويقدر له وما﴾ [سَبإ: 39]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Waambie, ewe Mtume, hawa waliodanganyika kwa mali na watoto, «Mola wangu anamkunjulia riziki Anayemtaka miongoni mwa waja Wake na Anambania Anayemtaka, kwa hekima Anayoijua. Na namna mtakavyotoa kitu chochote, Yeye Atawapa badala yake duniani na huko Akhera Atawapa malipo mema. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye bora wa wenye kuruzuku, basi tafuteni riziki Kwake Peke Yake na zungukeni kwa kufuata sababu zake Alizowaamuru |