Quran with Swahili translation - Surah Saba’ ayat 47 - سَبإ - Page - Juz 22
﴿قُلۡ مَا سَأَلۡتُكُم مِّنۡ أَجۡرٖ فَهُوَ لَكُمۡۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٞ ﴾
[سَبإ: 47]
﴿قل ما سألتكم من أجر فهو لكم إن أجري إلا على الله﴾ [سَبإ: 47]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, uwaambie wakanushaji, «Malipo niliyowaomba kwa wema huu niliowaletea ni yenu nyinyi. Malipo yangu mimi ninayoyangojea hayapo isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mwenye kuyaona matendo yangu na matendo yenu.Hakuna chochote kinachofichamana Kwake. Yeye Anawalipa wote: kila mmoja kwa anachostahiki.» |