×

Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii. 35:11 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah FaTir ⮕ (35:11) ayat 11 in Swahili

35:11 Surah FaTir ayat 11 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah FaTir ayat 11 - فَاطِر - Page - Juz 22

﴿وَٱللَّهُ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٖ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٖ ثُمَّ جَعَلَكُمۡ أَزۡوَٰجٗاۚ وَمَا تَحۡمِلُ مِنۡ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلۡمِهِۦۚ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٖ وَلَا يُنقَصُ مِنۡ عُمُرِهِۦٓ إِلَّا فِي كِتَٰبٍۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ ﴾
[فَاطِر: 11]

Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii. Kisha akakufanyeni mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote hachukui mimba, wala hazai, ila kwa ilimu yake. Na wala hapewi umri mwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake, ila yamo hayo katika Kitabu. Hakika hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: والله خلقكم من تراب ثم من نطفة ثم جعلكم أزواجا وما تحمل, باللغة السواحيلية

﴿والله خلقكم من تراب ثم من نطفة ثم جعلكم أزواجا وما تحمل﴾ [فَاطِر: 11]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na Mwenyezi Mungu Alimuumba baba yenu Ādam kwa mchanga kisha Akajaalia kizazi chake kitokamane na maji matwevu, kisha Akawafanya nyinyi ni wanaume na wanawake. Na hakuna mwanamke yoyote anayeshika mimba wala anayezaa isipokuwa Analijua hilo. Na hakuna mtu anayepewa maisha marefu au umri wake ukapunguzwa isipokuwa hayo yamo ndani ya Kitabu kilichoko Kwake, nacho ni Ubao Uliohifadhiwa, kabla mamake hajashika mimba yake na kabla hajamzaa. Hayo yote Mwenyezi Mungu Ameyadhibiti ameyajua kabla hajamuumba, hayataongezwa yale aliyoandikiwa wala hayatapunguzwa. Hakika kule kuwaumba nyinyi, kuzijua hali zenu na kuziandika kwenye Ubao Uliohifadhiwa ni jambo rahisi na sahali kwa Mwenyezi Mungu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek