Quran with Swahili translation - Surah FaTir ayat 10 - فَاطِر - Page - Juz 22
﴿مَن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡعِزَّةَ فَلِلَّهِ ٱلۡعِزَّةُ جَمِيعًاۚ إِلَيۡهِ يَصۡعَدُ ٱلۡكَلِمُ ٱلطَّيِّبُ وَٱلۡعَمَلُ ٱلصَّٰلِحُ يَرۡفَعُهُۥۚ وَٱلَّذِينَ يَمۡكُرُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ لَهُمۡ عَذَابٞ شَدِيدٞۖ وَمَكۡرُ أُوْلَٰٓئِكَ هُوَ يَبُورُ ﴾
[فَاطِر: 10]
﴿من كان يريد العزة فلله العزة جميعا إليه يصعد الكلم الطيب والعمل﴾ [فَاطِر: 10]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yoyote yule atakaye enzi ya duniani au Akhera, basi aitake kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na hilo halipatikani isipokuwa kwa kumtii Yeye, kwani enzi yote ni ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kujienzi na kiumbe, Mwenyezi Mungu Atamdhalilisha; na Mwenye kujienzi na Muumba, Mwenyezi Mungu Atamtukuza. Kwake Yeye utajo wake utapanda, na tendo lema Analiinua juu. Na wale wenye kutenda mabaya watapewa adhabu kali. Na vitimbi vya hao vitaangamia na vitaharibika na havitawafaidisha kitu chochote |