Quran with Swahili translation - Surah FaTir ayat 45 - فَاطِر - Page - Juz 22
﴿وَلَوۡ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِمَا كَسَبُواْ مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهۡرِهَا مِن دَآبَّةٖ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗىۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِۦ بَصِيرَۢا ﴾
[فَاطِر: 45]
﴿ولو يؤاخذ الله الناس بما كسبوا ما ترك على ظهرها من دابة﴾ [فَاطِر: 45]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau Mwenyezi Mungu Angaliwatesa watu kwa madhambi na maasia waliyoyatenda, Hangaliacha juu ya mgongo wa ardhi mnyama yoyote anayetembea juu yake. Lakini Anawapa muhula na Anachelewesha kuwaadhibu mpaka wakati maalumu Aliyoupanga. Na wakati wa kuwaadhibu ukija , basi Mwenyezi Mungu kwa waja Wake ni Mjuzi, hakuna yoyote kati yao atakayefichika Kwake, na hakuna chochote miongoni mwa mambo yao kilicho mbali na ujuzi Wake, na Atawalipa wao kwa walichotenda, chema au kibaya |