Quran with Swahili translation - Surah Ya-Sin ayat 28 - يسٓ - Page - Juz 23
﴿۞ وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَىٰ قَوۡمِهِۦ مِنۢ بَعۡدِهِۦ مِن جُندٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ ﴾
[يسٓ: 28]
﴿وما أنـزلنا على قومه من بعده من جند من السماء وما كنا﴾ [يسٓ: 28]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na jambo hilo halikuhitajia kuteremsha askari kutoka mbinguni ili kuwaadhibu wao baada ya wao kumuua yule mwanamume anayewapa ushauri mwema na kuwakanusha wajumbe wao, kwani wao ni wanyonge na watwevu zaidi kuliko kuwa ni wenye kufanyiwa hilo na hatukuwa ni wenye kuwateremsha Malaika tukitaka kuwaangamiza, bali tunawateremshia adhabu ya kuwavunjavunja |