Quran with Swahili translation - Surah Ya-Sin ayat 6 - يسٓ - Page - Juz 22
﴿لِتُنذِرَ قَوۡمٗا مَّآ أُنذِرَ ءَابَآؤُهُمۡ فَهُمۡ غَٰفِلُونَ ﴾
[يسٓ: 6]
﴿لتنذر قوما ما أنذر آباؤهم فهم غافلون﴾ [يسٓ: 6]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Tumekuteremshia wewe, ewe Mtume, ili uwaonye nayo watu ambao baba zao kabla yako wewe hawakuonya, nao ni Warabu. Watu hawa wameghafilika na wamepitikiwa na Imani na msimamo imara wa kufanya matendo mema. Na kila watu ambao uonyaji kwao umekatika, wanaingia kwenye mghafala na kupitikiwa. Katika haya kuna dalili ya ulazima juu ya wanavyuoni, wanaomjua Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kulingania na kukumbusha, ili wawaamshe Waislamu kutoka kwenye mghafala wao |