Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 124 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ نَقِيرٗا ﴾
[النِّسَاء: 124]
﴿ومن يعمل من الصالحات من ذكر أو أنثى وهو مؤمن فأولئك يدخلون﴾ [النِّسَاء: 124]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mwenye kufanya matendo mema, awe ni mwanamume au mwanamke, hali ya kuwa anamuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na haki Aliyoiteremsha, basi hao Mwenyezi Mungu Atawaingiza Peponi, nyumba ya starahe ya daima, na hawatopunguziwa chochote katika thawabu za matendo yao, hata kama ni kadiri ya kitone kilichoko kwenye koko ya tende |