Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 97 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَالُواْ فِيمَ كُنتُمۡۖ قَالُواْ كُنَّا مُسۡتَضۡعَفِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ قَالُوٓاْ أَلَمۡ تَكُنۡ أَرۡضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةٗ فَتُهَاجِرُواْ فِيهَاۚ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرًا ﴾
[النِّسَاء: 97]
﴿إن الذين توفاهم الملائكة ظالمي أنفسهم قالوا فيم كنتم قالوا كنا مستضعفين﴾ [النِّسَاء: 97]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika wale ambao Malaika waliwafisha na wao wako katika hali ya kujidhulumu wenyewe kwa kukaa katika nchi ya ukafiri na kuacha kuhama, Malaika watawaambia kwa njia ya kuwalaumu, «Mlikuwa katika nini kuhusu mambo ya Dini yenu?’ watasema, «Tulikuwa wanyonge nchini kwetu, tumelemewa kuweza kujiepushia dhuluma na maonevu.» Malaika watawaambia kwa njia ya kuwalaumu, «Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa kunjufu mkatoka kwenye ardhi yenu mkaenda ardhi nyingine ambapo mtaaminika na Dini yenu?» Basi hao makao yao ni Moto. Na haya ni makao mabaya ya mtu kuishilia |