Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 40 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿مَنۡ عَمِلَ سَيِّئَةٗ فَلَا يُجۡزَىٰٓ إِلَّا مِثۡلَهَاۖ وَمَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ يُرۡزَقُونَ فِيهَا بِغَيۡرِ حِسَابٖ ﴾
[غَافِر: 40]
﴿من عمل سيئة فلا يجزى إلا مثلها ومن عمل صالحا من ذكر﴾ [غَافِر: 40]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu katika uhai wake na akapotoka kwenye njia ya uongofu, hatalipwa huko Akhera isipokuwa mateso yanayolingana na maasia yake. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na akafanya matendo mema, kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake, awe mwanamume au mwanamke, na hali yeye ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na kumpwekesha, basi hao wataingia Peponi na humo Mwenyezi Mungu Atawaruzuku kutokana na matunda yake na starehe zake pasi na hesabu |