Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 85 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿فَلَمۡ يَكُ يَنفَعُهُمۡ إِيمَٰنُهُمۡ لَمَّا رَأَوۡاْ بَأۡسَنَاۖ سُنَّتَ ٱللَّهِ ٱلَّتِي قَدۡ خَلَتۡ فِي عِبَادِهِۦۖ وَخَسِرَ هُنَالِكَ ٱلۡكَٰفِرُونَ ﴾
[غَافِر: 85]
﴿فلم يك ينفعهم إيمانهم لما رأوا بأسنا سنة الله التي قد خلت﴾ [غَافِر: 85]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Imani yao hiyo haikuwa ni yenye kuwanufaisha walipoiona adhabu yetu, kwa kuwa ni imani ambayo hawakuwa na budi nayo, na si Imani ya hiyari na kutaka. Huo ndio mpango na njia Aliyoiweka kwa ummah wote, kwamba Imani isiwanufaishe wanapoiona adhabu. Na itakapokuja adhabu ya Mwenyezi Mungu, wataangamia wenye kumkanusha Mola wao, wenye kukataa kumpwekesha na kumtii |