Quran with Swahili translation - Surah Ash-Shura ayat 20 - الشُّوري - Page - Juz 25
﴿مَن كَانَ يُرِيدُ حَرۡثَ ٱلۡأٓخِرَةِ نَزِدۡ لَهُۥ فِي حَرۡثِهِۦۖ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرۡثَ ٱلدُّنۡيَا نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَا وَمَا لَهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ ﴾
[الشُّوري: 20]
﴿من كان يريد حرث الآخرة نـزد له في حرثه ومن كان يريد﴾ [الشُّوري: 20]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yoyote Anayetaka kwa matendo yake malipo mema ya Akhera, Akatekeleza haki za Mwenyezi Mungu na Akatoa katika kulingania Dini, tutamuongezea wema katika matendo yake, tumzidishie thawabu za jema moja mara kumi mpaka kipimo anachokitaka Mwenyezi Mungu cha nyongeza. Na yoyote yule Anayetaka kwa matendo yake ulimwengu peke yake, tutampa tulichomgawia cha huo ulimwengu , na hatakuwa na thawabu zozote huko Akhera |