Quran with Swahili translation - Surah Ash-Shura ayat 26 - الشُّوري - Page - Juz 25
﴿وَيَسۡتَجِيبُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضۡلِهِۦۚ وَٱلۡكَٰفِرُونَ لَهُمۡ عَذَابٞ شَدِيدٞ ﴾
[الشُّوري: 26]
﴿ويستجيب الذين آمنوا وعملوا الصالحات ويزيدهم من فضله والكافرون لهم عذاب شديد﴾ [الشُّوري: 26]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, wanamuitika Mola wao kwa kile Alichowaitia na wanajisalimisha Kwake, na Yeye Anawaongezea fadhila Zake kwa kuwaongoza na kuwazidishia malipo na thawabu. Na wale wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake watapata adhabu kali yenye kuumiza na yenye uchungu Siku ya Kiyama |