Quran with Swahili translation - Surah Az-Zukhruf ayat 20 - الزُّخرُف - Page - Juz 25
﴿وَقَالُواْ لَوۡ شَآءَ ٱلرَّحۡمَٰنُ مَا عَبَدۡنَٰهُمۗ مَّا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِنۡ هُمۡ إِلَّا يَخۡرُصُونَ ﴾
[الزُّخرُف: 20]
﴿وقالوا لو شاء الرحمن ما عبدناهم ما لهم بذلك من علم إن﴾ [الزُّخرُف: 20]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hawa washirikina wa Kikureshi wanasema, «Lau Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Angalitaka, hatungalimuabudu yoyote asiyekuwa Yeye.” Na hii ni hoja iliyotanguka, kwani Mwenyezi Mungu Ashasimamisha hoja juu ya waja kwa kuwatumiliza Mitume na kuteremsha Vitabu, basi kujisimamishia hoja ya Mapitisho na Makadirio ni ubatilifu mkubwa zaidi baada ya Mitume kuwaonya. Wao hawana ujuzi wa hakika ya yale wanayoyasema. Hakika ni kwamba wao wanayasema kwa kudhania na kuzua urongo, kwa kuwa hawana habari wala dalili kuhusu hilo kutoka kwa Mwenyezi Mungu |