Quran with Swahili translation - Surah Ad-Dukhan ayat 39 - الدُّخان - Page - Juz 25
﴿مَا خَلَقۡنَٰهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[الدُّخان: 39]
﴿ما خلقناهما إلا بالحق ولكن أكثرهم لا يعلمون﴾ [الدُّخان: 39]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hatukuviumba hivyo viwili isipokuwa kwa haki ambayo ndiyo mpango wa Mwenyezi Mungu katika kuumba Kwake na kupelekesha mambo Kwake. Lakini wengi wa hawa washirikina hawalijui hilo, na kwa hivyo hawavitii akilini vitu viwili hivyo, kwa kuwa wao hawatarajii kupata malipo mema wala hawaogopi mateso |